Տchool PVH
11K subscribers
297 photos
35 videos
900 files
924 links
The center of academic resources
📚 Primary School to teachers college

Android
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.schoolpvh

iOS
https://apps.apple.com/tz/app/school-pvh/id6445867210
📞
+255747272228
+255626272229
Download Telegram
Forwarded from INLINE LINKS
JIUNGE NA CHANNEL ZENYE MITIHANI KWA KULINGANA NA SOMO HUSIKA

Chagua somo lenye mitihani pia utaweza kujiunga na group kulingana na idara ya somo na kujadili pamoja👇👇👇👇Karibu
TAARIFA KWA UMMA
WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU
WA SHERIA MWAKA 2020


Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu
elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2020, kutoka
shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT
kwa mujibu wa Sheria.
Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi
watakayo kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa
kuripoti makambini kuanzia tarehe 24 hadi 27 Julai 2020.
Aidha, mafunzo hayo yatafunguliwa kuanzia 01 Agosti
2020.
Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi za JKT
Rwamkoma - Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu Pwani, JKT Mpwapwa Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT
Mlale - Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga,
JKT Makuyuni - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa,
na JKT Mtabila - Kigoma, JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa
na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na
JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.
Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho
(physical disabilities) waripoti katika kambi ya JKT Ruvu
iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya
kuhudumia watu wa jamii hiyo.
Aidha, kutokana na ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu
(COVID-19) Nchini, Tahadhari za kuzuia maambukizi ya
ugonjwa huo zitachukuliwa kipindi chote vijana
watakapokuwa makambini.
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa
vifuatavyo.
1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni
(lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu
unaoishia magotini, isiyo na zipu.
2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)
3. Raba za michezo zenye rangi kijani au blue.
4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye
baridi.
7. Track suit ya rangi ya kijani au blue
8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa
ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza
uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha
na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
Kuona orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa na
maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa bofya kwenye
jina la kambi hapo chini.