OPPORTUNITIES(unistoretz.com)
2.99K subscribers
196 photos
2 videos
52 files
1.5K links
✅ Matangazo Ya Ajira Tanzania
✅ Matangazo ya Scholarships-Fully Funded
✅ Matangazo ya Funding Opportunities-Fully Funded &Grants
✅ Nafasi za Internships
✅ Ujsariamali na Mawazo ya Biashara
✅ ELIMU

CONTACT unistoretz9@gmail.com
Download Telegram
NAFASI ZA KAZI KAMPUNI YA BECCO LIMITED TANZANIA


Ajira...

Elimu ya : Cheti cha Form Four
Elimu ya : Certificate
Elimu ya : Diploma
Elimu ya : Degree


wanahitajika

● Madereva
● mafundi Umemr
● Transport Officers
● Civil Engineers
● Archrectures
● Foremans
● Public Relations Officers
● Procurement Officers
● Mechanical Engineers
● Quantity Surveyors
● Human Resource Managers
● Security Officers
● Finance Officers
● Mechanic Technicians


Deadline: July 20,2019


Bonyeza Link-KUFAHAMU ZAIDI JINSI YA KU-APPLY
👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/jobs-opportunities-at-becco-limited/
WAZO LA BIASHARA

JUICE YA TENDE🥤🥤🥤

Hivi ushawahi Jiuliza Wapishi ni wengi Duniani, kuna Restaurants nyingi sana, kuna hotels nying sana Lakin UNAKUTA MAARUFU ZAIDI na watu wengi wanazozifahamu ni KFC, MacDonald, PizzaHut????

Yan Kitu wanachotengeneza ni Kile kile...lakin mtu ana Feel Proud akienda KFC😄....!! SIO UCHAWI...ILA NI BRANDING....


Unaweza ukauza ata mawe....na ukawa maarufu na ukatuboa..endapo utafanikiwa kwenye ishu ya BRANDING!!😃

Nisizungumzie sana maswala ya Branding.....embu Tuje kwenye mada yetu ya JUICE YA TENDE


Juisi ya Tende ni miongoni mwa juisi zilizojizolea umaarufu mkubwa hasa katika kurekebisha tatizo la nguvu za kiume.( Ina aminika sana hivo na jamii yetu hapa Bongo....kwasisi wajasiriamali TUNACHUKULIA KAMA OPPORTUNITY PA KOTOKEA SASA HAPO😄)


FAHAMU JINSI YANKUITENGENEZA

MAHITAJI :
- Tende kilo moja

- Maziwa ya unga au ya ng’ombe lita moja
- Sukari kiasi upendacho.

KUMBUKA : Tende zina asili ya sukari hivyo hakikisha unaweka kiasi

NAMNA YA KUTENGENEZA :
- Chukua tende zako kisha zitoe mbegu zake.

- Hakikisha unatoa mbegu tu na kuziacha tende kama zilivyo bila kutoa kitu kingine.

- Anza kuzisaga peke yake kwenye brenda hadi zitakapolainika sawasawa.

- Mimina maziwa yako kidogokidogo kwenye brenda ili kuzisaga vema jambo litakalosaidia juisi yako kulainika vema.

- Baada ya kutia maziwa yote na kuisaga sawasawa, tia sukari kiasi upendacho huku ukiendelea kuisaga ili sukari yako iweze kuchanganyika vizuri na juisi yako.
- Juisi yako itakuwa tayari kwa kunywa sambamba na kitafunwa chochote ukipendacho kama vile bagia, sambusa, korosho au karanga.


Inaendelea.....
UNAFANYAJE BIASHARA HII YA JUICE YA TENDE??? kwanini JUICE YA TENDE??🥤🥤


Ndio !! Juice ya Tende...Kwasababu sio watu wengi wanafanya hii biashara......

Yan ukizungumzia Biashara ya Juice hapa Bongo....Wengi wao wanauza hizi Juice common za matunda mengine.....kwahiyo wewe unaweza kuja Kivyako na Juice ya tende tuuh!!


KUHUSU MASWALA YA MTAJI na BUDGET !! Kiukweli hapo UTAJIPIMIA MWENYEWE..mimi sio.mtaalamu sana wa maswala ya fedha😄


Sasa ishu ipo kwenye BRANDING NA UNAIFANYEJE!!


Yan, ukitaka utoboe kwenye hizi biashara za juice....Lazima UFANYE BRANDING na UWE OFFICIAL!!

Branding.....nazungumzia

● Chagua Jina Zuri, Logo, Fungua social Media Accounts za biashara yako, Fungua website, na pia Fungua MOBILE APP ya watu ambayo wanaweza ku-Order Online


● Sajili Biashara Yako


● Sehemu Quality -Ofisi, ambayo utakuwa unatengenezea & Kuuza hiyo Juice ...

- Hapa ni kuchagua maeneo ambayo unajua utapata wateja (Kulingana na Wateja uliowalenga)


---->>> Watu wengi wanakimbiliaga maeneo ya Sheli za magari.....!! Ni vizur kama umetarget wateja wako ..LAKINI USIKARIRI!!!....

---->>> Biashara ya Juice unaweza fungua popote na UKAWA UNAFANYA DELIVERY KWENYE MAOFISI NA MAKAZI.MBALI MBALI!!!🚚🥤



● Usafi wa mazingira na bidhaa zako & Hakikisha ata unakuwa na Nutrianalist / Food Officer by Professional.....

- Hii itakusaidia sana kujemga uaminifu na wateja wako..kuwa unajali afya

● Packaging -- Yan Packaging iwe Quality...🥤🥤....Hakikisha Umeweka JINA na LOGO kwenye Package zako.....KUWA MBUNIFU SANA MAENEO hayo !!

Hizo ni baadhi ya Basic Tips tuuh...Mambo mengine Utajiongeza!!



KUHUSU WATEJA......



● Tatizo watu wengi tumekuwa tukiiga na kukariri.....Yan kwakuwa umeona watu wanauza JUICE maeneo ya sheli au Car wash....nawewe unataka KUFUNGUA MAENEO HAYO HAYO...!!


----->>>>> Embu Jaribu kuandaa Proposal & Presentation nzuri ya Biashara yako tafuta vijana wawili wanaojua Marketing vizuri....... PITENI MAOFISI MBALI MBALI hapo Mjini...Jaribu kutafuta soko uko!!!..........Pita kwenye mabenki, ofisi za makampuni mbali mbali, Pita ata kwenye maduka hapo town, Hadi Mahospitalini, Mashuleni, Ofisi za umma n.k......uwaelezee biashara yako!! Wape Offer siku mbili tatu......!! LAZIMA UTAPATA WATEJA TUUH!! TENA WATEJA WALE WA KUDUMU WA KILA SIKU KUWALETEA JUICE!!


------>>> uo ni mfano tuh, ila point ni ku- Tambua AINA YA WATEJA unaowahitaji na uwatafute!!!



Asanteni!!!


KWA MASWALI / MAREKEBISHO/ USHAURI

Wasiliana nasi

Email: unistoretz9@gmail.com
NAFASI ZA KAZI BENKI YA NMB


● Wanahitajika waliosomea Kozi za biashara

¤ Finance
¤ Account
¤ Economics
¤ Banking
¤ Business Administration
¤ Business Fields


Deadline: july 11,2019


Bonyeza link-APPLY ONLINE
👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/jobs-vacancies-at-nmb-bank-july-2019/
HABARI NJEMA KUTOKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI-NAFASI ZA SCHOLARSHIPS

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAMWAGA NAFASI ZA SCHOLARSHIPS KWA WATANZANIA-WANAFUNZI WOTE WANAOTAKA KUSOMA MASTERS 2020(SCHOLARSHIPS🇹🇿)
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

📣 🚨 UDHAMINI WA MASOMO-JUMUIYA YA AFRIKA MASHIRIKI( EAST AFRICAN COMMUNITY-EAC)

○ Baada ya Kuhitimu Utapata Fursa ya kupewa Internships/Mentorship&Training

✳ Jumuiya Ya Afrika Mashariki-YATANGAZA MASTERS SCHOLARSHIPS kusomea kozi hizi

● Kozi za Biashara-Business
● Engineering Fields
● Technology Fields
● Kozi zote za SCIENCE
● Mathematics Fields

Vigezo:

✅ Uwe Mtanzania
✅ Umri wako usizidi zaidi ya miaka 35 ( Below 35yrs of age)

Wanafunzi Wanaweza ku-Apply Chuo zaidi ya kimoja kati ya hivi

■ University of Nairobi
■ Kenyatta University
■ Makerere University
■ University of Dodoma
■ Dedan Kimath University
■ Instituit- Rwanda University
■ Sokoine University
■ MuCCOBS-Tanzania
■ Kubabii University

Deadline: August 01,2019

Bonyeza Link-APPLY ONLINE
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/call-for-applications-from-students-in-the-east-african-community-eac-to-pursue-kfw-funded-masters-scholarships/

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
NAFASI 146 ZA KAZI SHIRIKA LA AFYA-ELIZABETH GLASER PEDIATRIC AIDS FOUNDATION


● •Elimu kuanzia ya : Form Four+++

● • Elimu ya : Diploma, Nafasi za kazi

✳ NAFASI 146–Wanahitajika Vijana waliosomea kozi hizi

• Nursing
• Clinical Medicine
• Clinical Officers
• Community Health
• Business Administration
• Marketing
• Finance
• Public Administration
• Socialogy


Deadline: July 19,2019


Bonyeza Link-KUFAHAMU JINSI YA KU-APPLY
👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/146-jobs-at-ariel-glaser-pediatric-aids-healthcare-initiative-agpahi/
___________________________
NAFASI ZA KAZI VODACOM TANZANIA

wanahitajika Vijana waliosomea Kozi hizi:

• Business Administration
• Sales
• waliosomea sheria/Law
• Finance
• Marketing
• Other Business Fields

Deadline: July 15,2019

Bonyeza Link-APPLY ONLINE
👇👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/jobs-vacancies-at-vodacom-tanzania-limited/
________________________
WAZO LA BIASHARA



NJIA 5 ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA LITAKALOKUFANIKISHA



HABARI za wakati huu, nin­gependa kuanza na msemo kuto­ka wa Swami Vibekananda aliyenena; “Take up one idea. Make that one idea your life. Think of it, dream of it, live on that idea. Let the brain, muscles, nerves, every part of your body, be full of that idea and just leave every other idea alone. This is the way to success. That is way great spiritual giants are produced.”

Akimaanisha kama utaamua kuchukua wazo moja na kuliwaza, kulitafakari na kuwa ndilo kitu cha muhimu kwako, basi mwisho wa siku utafanikiwa. Kwa ufupi ni kuwa kila mtu mkubwa duniani alianza na wazo fulani lililomfani­kisha.

Iko hivi; yeyote ambaye huwa ana mawazo ya tofauti na yali­yotangulia kuliko wengine huwa anakuwa wa tofauti na atajikuta anapiga hatua kuliko wengine katika eneo lake. Aidha, uwe umeajiriwa, umejiajiri, mfanyabi­ashara, mwanasiasa au mwa­nafunzi; uwezo wako wa kuja na mawazo ya tofauti ndiyo kiini na chanzo cha mafanikio yako

 

1: TAFUTA UHITAJI


Kila mafanikio ni matokeo ya

uhitaji wa watu. Kila unacholi­pia pesa, kwako ni UHITAJI na kwa unayempa pesa ni kuwa AMETATUA TATIZO lako.

Kwa maneno mengine. Kadiri unavyoweza kutatua matatizo MAKUBWA na MENGI ndivyo unavyopata vyanzo vya pesa zaidi. Kwa ufupi umaskini ni matokeo ya kukimbia kutatua matatizo na utajiri ni matokeo ya kukimbilia kutatua matatizo.

Leo ningependa tuangalie njia kadhaa za namna ya kupata mawazo yanayoweza kuwa chanzo cha kubadilisha maisha yako unapoamua kuyafanyia kazi.

Na hapa ningependa kuwa­kumbusha maneno ya William Cameron aliyesema; “Money never starts an idea; it is the idea that starts the money.”

Fedha haileti mawazo ila ma­wazo ndiyo huleta pesa, ndiyo maana kuna watu walishawahi kupata pesa nyingi ila kwa ku­kosa mawazo wamerudi katika kufeli na umaskini.

Hebu chukua dakika moja, jiulize; Katika mazingira niliyopo, je, kuna uhitaji gani ninaoweza kuutatua? Chukua note book yako na andika kabla hatujaen­delea.

Hivyo basi angalia mazingira yanayokuzunguka, je, kuna uhitaji gani? Kama maji yana­toka mara moja kwa wiki mtaani kwenu, ukifanikiwa kununua simtank kadhaa na kuuza maji siku ambazo hayatoki hapo unakuwa umetatua tatizo na umepata pesa. Kama umeg­undua watu karibu na maeneo ya kwenu wanatumia gesi na hakuna duka la karibu, tafuta namna ya kuwa wakala wa kuuza, kadhalika na mahitaji mengine eneo ulilopo.

Naamini umepata mawazo kadhaa. Tutaendelea kujifunza kisha utabaki na wazo moja.

 

2: BORESHA WAZO LA MWINGINE

Kuna wakati mwingine hutahita­ji kuanza na wazo jipya kabisa, badala yake utahitaji kuchukua wazo la mwingine kuliboresha. Kwa mfano badala ya mtu kuuza matunda na kuyamenya mtu anaponunua mwingine ak­aboresha akaamua kuyamenya kabisa kisha anayapaki vizuri tayari kwa kuyauza.

Chunguza kile ambacho kina­fanywa na wengine kisha jiulize, hivi nawezaje kuliboresha wazo hili?

 

3: HAMISHA WAZO LA WEN­GINE NA LIPE UHALISIA WA MAZINGIRA YAKO

Kuna mawazo mengi yaliyofani­kiwa leo ni matokeo ya mawazo yaliyohamishwa kutoka mahali pengine na yakapewa uhalisia wa mahali husika. X-Factor ya Uingereza imezaa Bongo Star Search, DECA na SONY Records label ndiyo leo tunaona WCB.

Jaribu kuangalia, kuna wazo gani ambalo unaweza kuli­chukua na ukaliwekea mazin­gira ya kwako na ukalifanyia kazi. Unaweza kulitoa nje ya Tanzania na ukalileta Tanzania au ukalitoa Dar na ukalipeleka katika mkoa unaoishi.

 

4: RAHISISHA MCHAKATO WA KITU AMA BIDHAA FULANI

Sasa hivi kila mtu anajitahidi kutumia teknolojia kuuza bidhaa au kutoa huduma. Kwa nini? Kwa sababu ya kurahisisha mchakato kwa wateja.Tunaishi katika ulimwengu ambao watu hupenda kutumia muda mfupi kupata huduma au bidhaa, hivyo unachotakiwa kufanya ni kuhak­ikisha kuwa hata kama unatoa bidhaa au huduma ileile kama wengine, jaribu kurahisisha.

Ndiyo maana visimbuzi wanaweka huduma zao kwenye MPESA, Tigopesa, Airtel n.k, wanachojaribu kufanya ni kura­hisisha.

Inaendelea.....
Ni rahisi kwa mama ntilie anayepeleka chakula maofisini na akaongeza gharama ya us­afiri juu ya 500 kwa kila sahan

kuliko auze bei ya chini huku ak­isubiri watu wamfuate kilometa moja kule anakouza.

Inawezekana unataka ku­fanya kitu ambacho kila mtu anafanya, swali ni je, unaweza kutoa urahisi gani utakaovutia wanunuaji wa huduma au bid­haa yako?

 

5: TENGENEZA UHITAJI

Hii si njia rahisi sana ila in­awezekana. Inamaanisha kuna vitu vingi watu wanahitaji ila ha­wawezi kuvitumia hadi viwepo.

Kabla soda hazijaja watu wa­likuwa wanakunywa maji, kabla TV hazipo watu walikuwa ni radio tu na hakuna mtu alikuwa anadai TV kwa kuwa haiku­wepo. Lakini leo ni kama vile haiwezekani kuishi bila TV. Kuna mtu siku moja akauliza; “Hivi wazee wa zamani waliishije bila simu? Miahadi walifanyaje wakifika Kariakoo na kila mtu yuko kona yake?”

Hii ina maana kuna mahitaji mengi bado yako ila watu ha­wawezi kuyadai au kuulizia hadi yatakapokuwepo. Zamani scrub hazikuwepo ukienda saloon, lakini siku hizi ni kama vile ni lazima kila ukinyoa utajikuta unataka kufanya na scrub, tena ina bei kubwa kuliko hata kunyoa kwenyewe!

Hiyo inamaanisha kuna wazo unaweza ukaja nalo watu wakaanza kuhitaji hata kama hawajawahi kujua kama wana­hitaji.

 

HITIMISHO

Mawazo yako kila mahali, kiwango chako cha kujitoa kuy­atafuta na kuyafanyia kazi ndiyo kitu muhimu zaidi.

Kumbuka; kiwango chako cha kutengeneza mawazo mengi na kuyafanyia kazi ndiyo kitatege­mea utafanikiwa kwa kiwango gani katika maisha yako.


MAKALA HII IMEANDALIWA/ KUANDIKWA NA

©Joel Arthur Nanauka



Kwa maoni/ Ushauri/Marekebisho


Email: unistoretz9@gmail com
LAS VEGAS CASINO YAMWAGA NAFASI ZA KAZI KWA VIJANA


___________________________


Elimu ya: Form Four/Cheti cha 4m4


Wanahitajika Nafasi hizi:

✳ Wafanya Usafi wanahitajika

✳ Wasimamizi wa Bar Wanahitajika

✳ Waitresses Wanahitajika

✳ Walinzi wanahitajika

✳ Cashiers wanahitajika


Deadline: July 30,2019


Bonyeza Link-KUFAHAMU ZAIDI JINSI YA KU-APPLY
👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/jobs-opportunities-at-las-vegas-casino/
___________________________