OPPORTUNITIES(unistoretz.com)
2.99K subscribers
196 photos
2 videos
52 files
1.5K links
✅ Matangazo Ya Ajira Tanzania
✅ Matangazo ya Scholarships-Fully Funded
✅ Matangazo ya Funding Opportunities-Fully Funded &Grants
✅ Nafasi za Internships
✅ Ujsariamali na Mawazo ya Biashara
✅ ELIMU

CONTACT unistoretz9@gmail.com
Download Telegram
NAFASI ZA KAZI BENKI YA NMB


● Wanahitajika waliosomea Kozi za biashara

¤ Finance
¤ Account
¤ Economics
¤ Banking
¤ Business Administration
¤ Business Fields


Deadline: july 11,2019


Bonyeza link-APPLY ONLINE
👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/jobs-vacancies-at-nmb-bank-july-2019/
HABARI NJEMA KUTOKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI-NAFASI ZA SCHOLARSHIPS

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAMWAGA NAFASI ZA SCHOLARSHIPS KWA WATANZANIA-WANAFUNZI WOTE WANAOTAKA KUSOMA MASTERS 2020(SCHOLARSHIPS🇹🇿)
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

📣 🚨 UDHAMINI WA MASOMO-JUMUIYA YA AFRIKA MASHIRIKI( EAST AFRICAN COMMUNITY-EAC)

○ Baada ya Kuhitimu Utapata Fursa ya kupewa Internships/Mentorship&Training

✳ Jumuiya Ya Afrika Mashariki-YATANGAZA MASTERS SCHOLARSHIPS kusomea kozi hizi

● Kozi za Biashara-Business
● Engineering Fields
● Technology Fields
● Kozi zote za SCIENCE
● Mathematics Fields

Vigezo:

✅ Uwe Mtanzania
✅ Umri wako usizidi zaidi ya miaka 35 ( Below 35yrs of age)

Wanafunzi Wanaweza ku-Apply Chuo zaidi ya kimoja kati ya hivi

■ University of Nairobi
■ Kenyatta University
■ Makerere University
■ University of Dodoma
■ Dedan Kimath University
■ Instituit- Rwanda University
■ Sokoine University
■ MuCCOBS-Tanzania
■ Kubabii University

Deadline: August 01,2019

Bonyeza Link-APPLY ONLINE
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/call-for-applications-from-students-in-the-east-african-community-eac-to-pursue-kfw-funded-masters-scholarships/

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
NAFASI 146 ZA KAZI SHIRIKA LA AFYA-ELIZABETH GLASER PEDIATRIC AIDS FOUNDATION


● •Elimu kuanzia ya : Form Four+++

● • Elimu ya : Diploma, Nafasi za kazi

✳ NAFASI 146–Wanahitajika Vijana waliosomea kozi hizi

• Nursing
• Clinical Medicine
• Clinical Officers
• Community Health
• Business Administration
• Marketing
• Finance
• Public Administration
• Socialogy


Deadline: July 19,2019


Bonyeza Link-KUFAHAMU JINSI YA KU-APPLY
👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/146-jobs-at-ariel-glaser-pediatric-aids-healthcare-initiative-agpahi/
___________________________
NAFASI ZA KAZI VODACOM TANZANIA

wanahitajika Vijana waliosomea Kozi hizi:

• Business Administration
• Sales
• waliosomea sheria/Law
• Finance
• Marketing
• Other Business Fields

Deadline: July 15,2019

Bonyeza Link-APPLY ONLINE
👇👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/jobs-vacancies-at-vodacom-tanzania-limited/
________________________
WAZO LA BIASHARA



NJIA 5 ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA LITAKALOKUFANIKISHA



HABARI za wakati huu, nin­gependa kuanza na msemo kuto­ka wa Swami Vibekananda aliyenena; “Take up one idea. Make that one idea your life. Think of it, dream of it, live on that idea. Let the brain, muscles, nerves, every part of your body, be full of that idea and just leave every other idea alone. This is the way to success. That is way great spiritual giants are produced.”

Akimaanisha kama utaamua kuchukua wazo moja na kuliwaza, kulitafakari na kuwa ndilo kitu cha muhimu kwako, basi mwisho wa siku utafanikiwa. Kwa ufupi ni kuwa kila mtu mkubwa duniani alianza na wazo fulani lililomfani­kisha.

Iko hivi; yeyote ambaye huwa ana mawazo ya tofauti na yali­yotangulia kuliko wengine huwa anakuwa wa tofauti na atajikuta anapiga hatua kuliko wengine katika eneo lake. Aidha, uwe umeajiriwa, umejiajiri, mfanyabi­ashara, mwanasiasa au mwa­nafunzi; uwezo wako wa kuja na mawazo ya tofauti ndiyo kiini na chanzo cha mafanikio yako

 

1: TAFUTA UHITAJI


Kila mafanikio ni matokeo ya

uhitaji wa watu. Kila unacholi­pia pesa, kwako ni UHITAJI na kwa unayempa pesa ni kuwa AMETATUA TATIZO lako.

Kwa maneno mengine. Kadiri unavyoweza kutatua matatizo MAKUBWA na MENGI ndivyo unavyopata vyanzo vya pesa zaidi. Kwa ufupi umaskini ni matokeo ya kukimbia kutatua matatizo na utajiri ni matokeo ya kukimbilia kutatua matatizo.

Leo ningependa tuangalie njia kadhaa za namna ya kupata mawazo yanayoweza kuwa chanzo cha kubadilisha maisha yako unapoamua kuyafanyia kazi.

Na hapa ningependa kuwa­kumbusha maneno ya William Cameron aliyesema; “Money never starts an idea; it is the idea that starts the money.”

Fedha haileti mawazo ila ma­wazo ndiyo huleta pesa, ndiyo maana kuna watu walishawahi kupata pesa nyingi ila kwa ku­kosa mawazo wamerudi katika kufeli na umaskini.

Hebu chukua dakika moja, jiulize; Katika mazingira niliyopo, je, kuna uhitaji gani ninaoweza kuutatua? Chukua note book yako na andika kabla hatujaen­delea.

Hivyo basi angalia mazingira yanayokuzunguka, je, kuna uhitaji gani? Kama maji yana­toka mara moja kwa wiki mtaani kwenu, ukifanikiwa kununua simtank kadhaa na kuuza maji siku ambazo hayatoki hapo unakuwa umetatua tatizo na umepata pesa. Kama umeg­undua watu karibu na maeneo ya kwenu wanatumia gesi na hakuna duka la karibu, tafuta namna ya kuwa wakala wa kuuza, kadhalika na mahitaji mengine eneo ulilopo.

Naamini umepata mawazo kadhaa. Tutaendelea kujifunza kisha utabaki na wazo moja.

 

2: BORESHA WAZO LA MWINGINE

Kuna wakati mwingine hutahita­ji kuanza na wazo jipya kabisa, badala yake utahitaji kuchukua wazo la mwingine kuliboresha. Kwa mfano badala ya mtu kuuza matunda na kuyamenya mtu anaponunua mwingine ak­aboresha akaamua kuyamenya kabisa kisha anayapaki vizuri tayari kwa kuyauza.

Chunguza kile ambacho kina­fanywa na wengine kisha jiulize, hivi nawezaje kuliboresha wazo hili?

 

3: HAMISHA WAZO LA WEN­GINE NA LIPE UHALISIA WA MAZINGIRA YAKO

Kuna mawazo mengi yaliyofani­kiwa leo ni matokeo ya mawazo yaliyohamishwa kutoka mahali pengine na yakapewa uhalisia wa mahali husika. X-Factor ya Uingereza imezaa Bongo Star Search, DECA na SONY Records label ndiyo leo tunaona WCB.

Jaribu kuangalia, kuna wazo gani ambalo unaweza kuli­chukua na ukaliwekea mazin­gira ya kwako na ukalifanyia kazi. Unaweza kulitoa nje ya Tanzania na ukalileta Tanzania au ukalitoa Dar na ukalipeleka katika mkoa unaoishi.

 

4: RAHISISHA MCHAKATO WA KITU AMA BIDHAA FULANI

Sasa hivi kila mtu anajitahidi kutumia teknolojia kuuza bidhaa au kutoa huduma. Kwa nini? Kwa sababu ya kurahisisha mchakato kwa wateja.Tunaishi katika ulimwengu ambao watu hupenda kutumia muda mfupi kupata huduma au bidhaa, hivyo unachotakiwa kufanya ni kuhak­ikisha kuwa hata kama unatoa bidhaa au huduma ileile kama wengine, jaribu kurahisisha.

Ndiyo maana visimbuzi wanaweka huduma zao kwenye MPESA, Tigopesa, Airtel n.k, wanachojaribu kufanya ni kura­hisisha.

Inaendelea.....
Ni rahisi kwa mama ntilie anayepeleka chakula maofisini na akaongeza gharama ya us­afiri juu ya 500 kwa kila sahan

kuliko auze bei ya chini huku ak­isubiri watu wamfuate kilometa moja kule anakouza.

Inawezekana unataka ku­fanya kitu ambacho kila mtu anafanya, swali ni je, unaweza kutoa urahisi gani utakaovutia wanunuaji wa huduma au bid­haa yako?

 

5: TENGENEZA UHITAJI

Hii si njia rahisi sana ila in­awezekana. Inamaanisha kuna vitu vingi watu wanahitaji ila ha­wawezi kuvitumia hadi viwepo.

Kabla soda hazijaja watu wa­likuwa wanakunywa maji, kabla TV hazipo watu walikuwa ni radio tu na hakuna mtu alikuwa anadai TV kwa kuwa haiku­wepo. Lakini leo ni kama vile haiwezekani kuishi bila TV. Kuna mtu siku moja akauliza; “Hivi wazee wa zamani waliishije bila simu? Miahadi walifanyaje wakifika Kariakoo na kila mtu yuko kona yake?”

Hii ina maana kuna mahitaji mengi bado yako ila watu ha­wawezi kuyadai au kuulizia hadi yatakapokuwepo. Zamani scrub hazikuwepo ukienda saloon, lakini siku hizi ni kama vile ni lazima kila ukinyoa utajikuta unataka kufanya na scrub, tena ina bei kubwa kuliko hata kunyoa kwenyewe!

Hiyo inamaanisha kuna wazo unaweza ukaja nalo watu wakaanza kuhitaji hata kama hawajawahi kujua kama wana­hitaji.

 

HITIMISHO

Mawazo yako kila mahali, kiwango chako cha kujitoa kuy­atafuta na kuyafanyia kazi ndiyo kitu muhimu zaidi.

Kumbuka; kiwango chako cha kutengeneza mawazo mengi na kuyafanyia kazi ndiyo kitatege­mea utafanikiwa kwa kiwango gani katika maisha yako.


MAKALA HII IMEANDALIWA/ KUANDIKWA NA

©Joel Arthur Nanauka



Kwa maoni/ Ushauri/Marekebisho


Email: unistoretz9@gmail com
LAS VEGAS CASINO YAMWAGA NAFASI ZA KAZI KWA VIJANA


___________________________


Elimu ya: Form Four/Cheti cha 4m4


Wanahitajika Nafasi hizi:

✳ Wafanya Usafi wanahitajika

✳ Wasimamizi wa Bar Wanahitajika

✳ Waitresses Wanahitajika

✳ Walinzi wanahitajika

✳ Cashiers wanahitajika


Deadline: July 30,2019


Bonyeza Link-KUFAHAMU ZAIDI JINSI YA KU-APPLY
👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/jobs-opportunities-at-las-vegas-casino/
___________________________
WAZO LA BIASHARA


JINSI YA KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUTUMIA MATANGAZO YA "sponsored Ads"


Uishawahi pita pita uko Instagram au facebook ukaona "SPONSORED ADS" ???

Leo nataka nikuelezee jinsi ya Ku-Boost matangazo hayo kupitia FACEBOOK na INSTAGRAM


"FACEBOOK INALIPA SANA" Hii nitaelezea siku nyingine JINSI YA KUTENGENEZA PESA KUPITIA FACEBOOK !!👌


Sasa mimi nawashangaaga sana unakuta mtu anakwambia FACEBOOK ya washamba😄😄... na anajisifia kabisa eti hana Facebook Account !!! Namimi najiulizaga sijui ana-Survive vp?..anyways !! tuyaache hayo....


Kila mtu majua Facebook ni moja wa mtandao wa kijamii unaokutanisha watu katika kushea maandiko,picha,videos n.k


Mtandao huu wa Facebook ulianzishwa mnamo mwaka 2004 na mwanafunzi wa chuo kikuu cha Harvard, ajulikanaye kwa jina la Mark Zuckerberg na kipindi hicho ulikuwa unatumiwa na wanafunzi tu kwa ajili ya kujadili juu ya masomo yao, lakini baadae uliweza kukuwa zaidi na kuruhusu hata watu wa kawaida kutumia mtandao huo.


SASA LEO WACHA NIKUELEZEE KUHUSU SPONSORED ADS



Natumia lugha nyepes sponsored ads inayofahamika ila kwenye facebook utaona option inaitwa "ADS MANAGER"
au "PROMOTIONS"


VITU MUHIMU VYA KUWA NAVYO ILI UWEZE KU-PROMOTE KUPITIA FACEBOOK NA INSTAGRAM


1⃣ Lazima uwe na FACEBOOK ACCOUNT iliyokamilika ( yan uwe umejaza taarifa zako zile muhimu kwa profile yako)

¤ Sasa hapa hii Account yako.
ukishakuwa nayo utafungua account ingine ya Facebook ndab ya iyo iyo account yako -BUSINESS FACEBOOK ACCOUNT


2⃣ Lazima uwe na Account number ya Bank / Card ya Bank yenye pesa


3⃣ Lazima uwe na Instagram Account ( Business Instagram Account)


JINSI YA KUUNGANISHA NA KUWEZESHA ACCOUNT ZAKO ZIWEZE KU-PROMOTE

1⃣ Baada ya kuingia kwenye facebook account yako....



¤ Unatakiwa Kufungua BUSINESS FACEBOOK ACCOUNT.......ambapo utaingia
👇👇👇👇👇👇👇👇
business.facebook.com

¤ Ukishaingia hapo utafungua account yako ingine ya biashara ambayo ni maalumu kwa ajili ya matangazo

¤ Ukishaingia hapo utabonyeza Option ya "CREATE ACCOUNT"


¤ Alafu utachagua option ya ADS MANAGER - ambapo utaweza tengeneza Tangazo lako


2⃣ Tengeneza Facebook Page kulingana na Aina ya biashara yako....

¤ iyo facebook page----Utaona sehemu ya ku-Link Page yako ya facebook na instagram account!! Hapo LINK, NI MUHIMU SANA!


3⃣ Ukisha Fungua Business Account yako...Tafuta option kwenye uko uko Business for facebook sehemu pameandikwa "PAYMENT SETTINGS" ingia hapo.....Jaza taarifa zako za MALIPO



KUMBUKA: KADI YAKO YA BENKI NI LAZIMA IWE IMEWEZESHWA NA BENKI HUSIKA KUFANYA MALIPO ONLINE !! NENDA BENKI YAKO, WAAMBIE WAWEZESHE KADI YAKO.KUFANYA MALIPO ONLINE!! wataiwezesha



● Utajaza Account number yako na taarifa za kadi yako ya Benki

● Utachagua aina ya malipo kulingana na unavyopenda ( Msater Card /Visa Card/paypal n.k)

● utalipia kiasi cha pesa ambacho ungependa kuspend kama Budget yako ya Promotion




ITAENDELEA........
BAADA YA KUTENGENEZA HIYO BUSINESS MANAGER


KESHO NITAELEZEA JINSI YA KUTENGENEZA TANGAZO AMBALO NDIO SPONSORED AD


NA JINSI YA KUSET BUDGET...NA TIPS MUHIMU KATIKA KUPROMOTE BIASHARA YAKO KUPITIA FACEBOOK /INSTAGRAM


Yani huku .....UNAWEZA TANGAZA BIASHARA YAKO ATA kwa $1 kwa siku tuuh ....SIO BEI KUBWA KAMA WATU WANAVYODHANI HADI WANAOGOPA.....NI BUDGET yako mwenyewe unachagua!!


©Makala imeandaliwa na kuandikwa na Unistoretz Inc


ITAENDELEA KESHO.......

Kwa maoni /Ushauri / Marekebisho....Msaada /

Wasiliana nasi
👇👇👇👇👇
Email : unistoretz9@gmail.com
NAFASI 19 ZA KAZI MORUWASA


Elimu ya 4m4/Certificate


Wanahitajika:

● Assistant Technicians
● Pump Operators
● Human Resources
● Plumbers
● Wasomaji Meters


Deadline" July 23,2019


Bonyeza Link-KUFAHAMU JINS YA KU-APPLY
👇👇👇👇👇👇👇👇
http://www.unistoretz.com/magazine/19-jobs-vacancies-at-moruwasa-july-2019/